Wednesday, 28 September 2016

Handmade, bidhaa asilia toka Tanzania...

Twitter: @CarolAnande Instagram: @CarolAnande Facebook: @CarolAnande


Kwenye anga zangu za ulingo wa Sanaa, nimekutana na wadau wengi wa biashara za kazi ya mikono Tanzania. Ambao wanatoa ajira haswa kwa wanawake pia vijana na walemavu, Tanzania. Chini ni baadhi ya biashara hizi, nazodhani ni vyema ziungwe mkono...


Pili Hassan Maguzo ni mjasiriamali biashara yake Pili's, Aliianza tangu mwaka 2014 alipojaribu kuangalia nini anaweza kuuza pale Coco Beach. Aliona hamna wauzaji wa juisi ya miwa, hivyo akafanya juhudi mpaka akaanza kuuza juisi hiyo. Hivi leo Pili's huonekana kwenye maonyesho mbalimbali kama kibanda cha chakula chenye juisi, saa ingine mihogo hata 'cocktails'. Pili's imeajiri watu saba toka Tanzania (0762 524 781) 
Pili's 
Pili's 

Dada Abir Ibrahim (Public Health) toka Sudan mara yake ya kwanza Tanzania, akiwa anafanya kazi za 'kujitolea'. Alikutana na wanawake vijijini waliomgusa kwa kuwa walikuwa hawana kipato. Alijua hakuweza kuzidi kuwaajiri wote kwa vikazi vidogo vidogo vya nyumbani, na vivyo INUA ikazaliwa.. INUA leo inatoa huduma ya bidhaa za nywele na ngozi, zenye malighafi asilia kama mafuta ya nazi, mchachai, parachichi, shea butter na kadhalika vingi vikitoka Tanzania. INUA imeajiri wanawake wa Tanzania wengi wakitokea Tanga na Dar es Salaam (0757 446750) 
INUA Naturals
INUA Naturals

Ma 'Lydia Jacob' akiwa mbele ya bidhaa zake toka 'Upendo Food Processors'. Kiwanda chao kipo mkoa wa Pwani-Kisarawe. Kikundi kipo na watu kama saba hivi wakiwaajiri vijana na wanawake toka vijiji majirani. Bidhaa zao zinapatikana Dar es Salaam ndani ya 'Shirji Supermarket', Mbezi Madukani Terminal one. (0784 807 450)
Bidhaa za 'Upendo Food Processors'
Bidhaa za 'Upendo Food Processors'


Fahari ni 'NGO" ambaye ilianzishwa na Julie Lawrence, Mama anayetokea Wingereza aliyebobea kwenye ubunifu wa 'accesories' kwa miaka mingi ulaaya. Alianzisha FAHARI kwani aliona fursa ya kutoa ujuzi wake kwa wanawake tokea Zanzibar, ambao kwa kawaida hawangepata ujuzi huo kiurahisi. Mpaka sasa FAHARI imetoa mafunzo kwa wanawake zaidi ya 50, 14 ya hawa wameajiriwa na FAHARI. Duka lao lipo 'Mji Kongwe Zanzibar' 62, Kenyata rd, likiwa na bidhaa mbalimbali za ngozi na ukili, pamoja na 'canvas' na 'shells' malighafi haya yakitokea Tanzania. (0776 514 949) 
Bidhaa ya FAHARI
Bidhaa za FAHARI
Bidhaa ya FAHARI

'Jina Langu Ni...' wanatengeneza mikufu, bangili, mikanda, vipuli na bidhaa kama hizi kutokana na Khanga na Vitenge. Ni 'NGO" inayowapa ajira kina mama wenye ulemavu tokea Dar es Salaam. Ilianzishwa mwaka 2011, ikiwa na Mbunifu wa 'Accesories' Dada Deny Grillo (kwenye picha hapa) tokea Italy.  Vivyo huwa anatoa mafunzo kwa hawa kina mama tokea Tanzania, ambapo wanaohitimu huaajiriwa kutengeneza bidhaa hizi. (0787 442 100)


'Neema Crafts' ni 'NGO" likiwa na zaidi ya miaka 10, lilianzishwa na Dayosisi ya Ruaha. Mpaka sasa inasiaidia na kuajiri zaidi ya watu 100, wenye ulemavu Iringa. Ikiwa na 'Mkahawa', Miradi 8 ikitengeneza bidhaa mbalimbali za mikono.  Pia ina sehemu ya mkutano, 'guesthouse' na  natoa misaada nsaha kwa watoto walemavu (orders@neeemacrafts.com)
Bidhaa za Neema Crafts

'Mama Masai' ilianzishwa mwaka 2000 ni mtandao wa vikundi 15.  vinavyo jitegemea na kushirikisha zaidi ya wanawake 150 wa jamii ya Kimasai. Bidhaa zao zinahusisha ubunifu wa jamii kwenye shanga na ngozi, wana duka pale Oysterbay Kaunda Drive 22/6 (0653 113 692)
Bidhaa za 'Mama Masai

Vikapu Bomba ni biashara ya kijamii inayofanya kazi na wanawake wa kijiji cha Lulanzi kule Iringa, 'Vikapu Bomba' inawapa nafasi ya kujifunza jinsi ya kuendesha biashara ndogogo na jinis ya kushona vikapu vyeye kuvutia zaidi. Kila kikapu kinakuja na jina ya mama aliyekishona ili mteja ujue ni nani unayemuinua kwa kushiriki na kutumia bidhaa hizi (vikapubomba@gmail.com 0759 548 581)
Bidhaa ya Vikapu Bomba

 WomenCraft ni shirika la jamii linalotengeneza bidhaa za nyumbani kwa kazi za mikono za wanawake tokea Burundi, Tanzania na Rwanda. Makao makuu yake ni Ngara, kwenye milima ya 'Mafiga Matatut' Tanzania. Inafanya kazi na zaidi ya wanawake 300 ambao wamebobea kwenye usukaji wa majani mbalimbali kama ukili. INtamvi na Ugwafu.Bidhaa zao husafirishwa ndani na nje ya nchi (0732 983 150)

Bidhaa za WomenCraft

Changamoto ni shirika la NGO lenye makao Tegeta Dar es Salaam, wao wameona jinsi ya kuwasaidia wanawake na wanaume ambao wameathirika na madawa ya kulevya na pombe. Kwa kuwalipia ushauri fashaha, kwa kuwahusisha na kazi za mikono, kama za ufundi seremala, uchomaji vyuma na kazi zingine za mikono kama hizi. Wanatoa huduma ya 'counselling' kwa wanawake pita 0712 56 87 73 na kwa wanaume pita 0783 41 31 38...Kwa kuchangia shirika hili kwa kunua bidhaa zao info@changamoto.org
Bidhaa za Changamoto
Bidhaa za Changamoto

Wonder Workshop ni NGO inayofanya kazi na walemavu ikitengeneza sanaa rejereshi. Kutokea vyakula ambapo wanatengeneza karatasi za kadi, album nakadhalika. Pia mabaki ya miti wanayotengenezea toyi za kuchezea watoto, pia vyuma vibovu wao huvabadilisha kuwa sanaa za kuchonga na vifaa vingine adilifu. Mradi wao uko pale Oysterbay Dar es Salaam (1372 Karume Rd-0754 051 417)
Bidhaa za Wonder Workshop
Bidhaa za Wonder Workshop

'Sanaa Tamu'  ni kampuni ya Mtanzania inayotengeneza bidhaa za mbao zenye ubunifu wa hali ya juu. Nyingi ya bidhaa zao zinatokana na mabaki ya 'dau' vivyo ni nzito na za kudumu. Na zote zinatengenezwa na mikono (0713 414 270)
Bidhaa za Sanaa Tamu
Bidhaa za Sanaa Tamu

Mwakilishi toka AFRICRAFT akiuza bidhaa zao, AfriCraft imekuwa ikiendesha biashara tangu mwaka 2005. Mpaka sasa inafanya kazi na mafundi wa kazi za mikono takribani 120, ndani na nje ya Dar es Salaam. Kutoka vyakula, bidhaa za miti na glasi. AfriCraft inajali mazingira vivyo bidhaa zao nyingi, zimerejereshwa nyingi toka kwenye taka taka kama plastiki. (0782 394 302)
Bidhaa za AfriCraft

Sweet Rebel Home Bakes, ni kampuni ya LeAnne Pollock na mwenzi wake Ambrose Akwabi ikiwa na makao makuu pale Slipway' Dar es Salaam. Huuza bidhaa za kuokwa kama mikate, keki, 'pies' na vingine vitamu, malighafi zao zote kutoka ngano mpaka samli na jibini zimetokea Tanzania (0712 507 075)
Bidhaa za 'Sweet Rebel Home Bakes'


Nilikutana na Babu Suleiman kwenye onyesho la Farmers Market pale Oysterbay, kwenye meza yake alikuwa na vitu vizuri. Haswa mafuta mbalimbali ya asilia kama mafuta ya mkaratusi, mchai chai, safarani, ubuyu nakdhalika. Anapatikana (0777 859 457)

Hizi ni bidhaa za Boma Group nao niliwabamba kwenye onyesho la kila mwezi 'Farmers Market' pale Oysterbay Shoping Centre, Dar es Salaam. Ni kikundi cha watanzania kinachoajiri vijana na wanawake watanzania (0756 360 657)
Bidhaa za Boma Group

Hawa kina mama wanatokea kikundi cha 'Tanzania Disabled Culture Group' , wanauza bidhaa zao pale Machinga Complex, Dar es Salaam
 (0652 260 994)

1 comment:

  1. Mm nabandika shanga kwenye mikanda je tunaweza kufanya biasha,,yani nashona nyinyi mnanunua kuongeza wigo wa biashara yenu.

    ReplyDelete