Tuesday, 3 October 2017

The man who coined 'Swahili Blues'


Leo Mkanyia on his guitar with Swahili Blues member
in the background 'Jose' playing drums
with a curious mix of the 'makonde'
'mtonya' drum
Sio kitu rahisi kutumbua tanzu mpya ya muziki, lazima uwe na uzoefu wa kupiga ala mojawapo au kadhaa za muziki, kama gitaa au sauti. Vivyo uwe na uzoefu wa kupiga tanzu nyingine za muziki kwani ubunifu huchukua malighafi yaliyopo na kutotoa kitu kipya. Kwa mfano tanzu ya muziki wa ‘blues’ iliyotungwa na Wamerikani Weusi kwenye miaka ya 1920’s, ndo iliyo zaa tanzu za ‘rock n roll’ pamoja na ‘r&b’ ambayo kirefu chake ni ‘rhythm na blues’.

Hapa tupo na Leo Mkanyia mwanamziki tokea Tanzania, mtoto wa Henry Mkanyia mwanamziki mkongwe aliyepiga muziki kwenye bendi ya ‘Mlimani Orchestra Park’ iliyotamba miaka ya 80.

Leo miaka ya 2010, alitumbua tanzu mpya ya muziki, kwa usaidizi wa baba yake. Aliipa jina la ‘Swahili Blues’ na vivyo kuwa jina la bendi yao. Tanzu hii imechanganya vionjo vya muziki wa Tanzania kama sikinde, ‘Afro beat’ na ‘blues'.
The percussionist in 'Swahili Blues' band Kilima
working his magic with djembe, congas... 
Nilikumbana na Leo akiwa tayari kupanda jukwaani pale Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa na bendi yake swahli blues. Huwa wanapiga pale Serena Hotel jijini Dar es Salaam, kila Ijumaa kuanzia saa moja hadi saa nne usiku.

Wengine kwenye bendi hii ni pamoja na baba yake Henry akichapa gitaa la ‘base'. Kilima yeye hupiga ngoma mchanganyiko kama djembe, conga na ‘chimes’ seti yake ilinifurahisha sana. Usiku huu pia Jose anayepiga ngoma za vyuma alikuwepo kwenye bendi na yeye mchanganyiko wake wa ngoma hizi na ngoma ya Tanzania ya 'mtonya' ulinikuna moyo.

Leo Mkanyia kama muwakilishi wa bendi hii ana albamu tatu kwenye kapu lake. Ya kwanza ni albamu fupi ‘dunia hii’, aliyoizindua rasmi mwaka 2010; ya pili ni ‘dunia hii’ hii ikiwa albamu kamili iliyotoka mwaka 2011. Mwaka jana alizindua albamu yake mpya ‘Bangili’ kule Kenya. Albamu mbili za kwanza alizi rekodi kwa kujitegemea, ni albamu hii ya ‘Bangili’ alipobebwa na ‘Ketebul Music’ kampuni ya muziki toka Kenya http://www.ketebulmusic.org.

Leo mpaka sasa ana takribani miaka 15 kwenye muziki, 10 akiwa kikamilifu kwenye fani hii. Ameshafanikiwa kupiga mikoani Tanzania pamoja na jukwaa mbali mbali nje ya nchi. Kama Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Uingereza, Ethiopia, kwenye matamasha kama Bayimba, Sauti za Busara na 'London African Music'. Kwenye nyimbo zake anatumia lugha ya Kiswahili, kilugha na vionjo vya Kifaransa na kiingereza.

Nilimuuliza nini siri ya mafanikio yake haswa ukizingatia muziki wa aina ya moja kwa moja, unasuasua nchini. 

Henry Mkanyia Leo's father a veteran musician
prominent in his time with 'Mlimani Orchestra Park'
and now with his son in 'Swahili Blues'
Alinijibu “muziki una maisha fulani ambayo unachagua, ukitaka kuishi ki ‘star’ unaweza. Ukitaka kuishi kawaida kabisa kama sisi unaweza… mwisho wa siku kufanya kazi kwa bidii na kuwa na malengo ni muhimu sana. Watu wengi wanapoteza malengo baada ya kufuata mambo ya hapa na pale, shida za hapa na pale wanapoteza dira.

Vikundi vingi vimekufa watu wanapoteza malengo, sasa hivi ukiangalia hapa Dar es Salaam tofauti na miaka mitatu iliyopita bendi nyingi zinafifia…Muziki si mazoezi tu, mazoezi ni  sehemu ya muziki. Inabidi pia uimarishe mitandao yako kwasababu leo wanamziki waliofanikiwa. Sio wote wana kipaji kikubwa, ila wana mitandao mzuri. Hifadhi ‘contacts’, fanya kazi na watu vizuri leo unawahitaji kesho watakuhitaji…” Leo Mkanyia
Ukitaka kujipatia albamu za Leo Mkanyia tembelea duka la vitabu la ‘Novel Idea’ kwenye matawi yake mbalimbali http://anovelidea.co.tz. Vinginevyo waweza sikiliza nyimbo zake na kuzinunua ‘online’ kupitia tovuti yake https://leomkanyia.com/listen/

Well if in Dar es Salaam and your looking to hear some seasoned music that is latent with a bluesy essence mixed with traditional Tanzanian rhythms. Pop by at Serena Hotel on Friday night at their bar, Swahili Blues have been performing here for now 5 years. I captured a whiff of their tune on video here <iframe src="https://www.facebook.com/plugins/video.php?href=https%3A%2F%2Fwww.facebook.com%2FCarolAnande%2Fvideos%2F1485495198213739%2F&show_text=0&width=560" width="560" height="315" style="border:none;overflow:hidden" scrolling="no" frameborder="0" allowTransparency="true" allowFullScreen="true"></iframe>

By +Caroline Anande Uliwa @CarolAnande-Instagram @CarolAnande-Facebook @CarolAnande-Twitter

No comments:

Post a Comment