Wanadansi akwemo Tiko Mbepo ( mwisho kulia) tokea Tanzania |
“Yani hili janga likiisha wengine tutabidi tupimwe
kisaikolojia, manake saa ingine unadhani una ugonjwa kumbe ni ‘stress’…”Remi
Tone mwanamziki na mjasiriamali kwenye sekta ya muziki wa jukwani akijibu jinsi
gani janga la Corona limeathiri kazi zake.
Tangu Corona itie mguu Tanzania mnamo mwezi Machi mwaka
huu, sekta ya utamaduni na sanaa imeathirika kwa kiasi kikubwa. Hapa tumeongea
na wadau mbali mbali kwenye sekta hii akiwemo Katibu Mtendaji wa BASATA Bw
Godfrey Mngereza, na wasanii wasiopungua kumi ili kubaini hali halisi na suluhu
gani zinazojitokeza kwa sekta hii kwa kipindi hiki.
Changamoto
“Ratiba yangu yote mwaka huu imetibuliwa ndani na nje ya
nchi, nilikuwa natarajia kwenda kikazi mwaka huu South Afrika, Bolivia,
Wingereza, Japan, Ghana na Eygpt ila mwishowe nilianza kuzoea ile barua pepe
yenye ujumbe ‘Tunasikitika kukuarifu tumesitisha…” huwa nafundisha
mashuleni na kwa watu wazima ila hadi
sasa hizi kazi pia zimesitishwa.” Dada Mwandale Mwanyekwa mwalimu na mkufunzi
wa Sanaa ya ufundi hususani uchongaji wa vinyago alielezea.
Mwandale Mwanyekwa ama Big Mama mkali wa sanaa za ufundi TZ |
Tulivyongea na Bw Robert Mwampemwa mkurugenzi wa chama
cha wasanii wa ufundi ‘Tanzania Visual Artists Association’ yeye pia
alishuhudia kuwa hali sio nzuri kwa wasanii wengine kwenye tasnia yake. Alisema
kwa ajili sekta nyingi za uchumi zimeathirika kama vile utalii basi “Mnyororo
wa uzalishaji umeathirika mno, mfikirie yule Mama Iringa anayesuka vikapu leo
hii anashindwa kumuuzia yule mchukuzi aliyetoka mjini kwani yule haoni soko na
vivyo hanunui kazi yake.”
kazi ya dada Jamila Vera Swai mmoja wa wanachama wa TFDA |
Bwana Robert aliongezea kwa kusema vikundi vya
uzalishaji wa hizi rasilimali za kazi za ufundi, wengi wao waliokuwa wakitoa
ajira kwa vijana na watu wasiojiweza.Sasa wamebidi waachishe kazi wafanya kazi
wao. Na kuwarejesha kwenye majaribio ya pombe na madawa ya kulevya.
Hili swala la kazi kukauka kwenye sekta hii lilikuwa jibu kutoka kwa wasanii wengi tuliongea nao hapa. Wengine wakiwa madansa, wanamuziki, wabunifu wa mavazi, wanafilamu. Swala la kusitishwa kwa mikusanyiko ya hadhara pia nchi ngeni kufunga mipaka yao ama kuwepo kwenye mifungo wa ndani yani ‘lockdowns’.
Kumeathiri wasanii kwa karibu kabisa “Ukisitisha
matamasha, harusi, ‘kitchen party’, na hafla nyingine unaathiri biashara zetu
moja kwa moja. Kwani hawa ni wateja wetu ambao wangeshona mavazi yao kwetu” Bw
Ndesumbuko Merinyo mkongwe kwenye sekta ya ubunifu wa mavazi nchini, na jina la ‘Afrika Sana’; pia ni mkuu wa ‘Tanzania Fashion Designer Association-TAFDA
tafda.org Alitujulisha hali halisi ya wanachama wake ndani ya tasnia hii, jinsi
wanavyokabiliana na Corona.
Aliongezea kwamba wengine wamebidi wawachishe
mafundi wao kazi, kwani vyumba vya kazi walivyonavyo ni vidogo na kutokimu
taratibu za kukaa mbali zinazopendekezwa kwenye kujitahadhari na Corona.
kazi ya Bw Thobias Minzi ama Minzi Mims mkufunzi na mmoja wa wanachama wa TVAA |
Madansa pia wameathirika kama mwana dansa Tiko Mbeko
alivyotuarifu, yeye ni mkuu wa kikundi cha T-Africa tafricadancecrew. Na wao
wamejikuta kazi zao ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam zikisitishwa.
Hata sekta ya uchapishaji nayo imeathrika, “Unajua pato
limepungua kwa namna kadhaa kufikia hadi asilimia 80. Ndio hiki kitabu kipya (Development as Rebellion-Wasifu wa Mh Julius
K. Nyerere) kimetoa muamko kidogo. Ila mwishowe hatutegemei mauzo ya kitabu
kimoja…kwa saa kuna watu wachache mjini ambako duka letu lipo” Mkuki Bgoya wa
kampuni ya uchapishaji Mkuki na Nyota, wenye duka la vitabu TPH BookStore. Alielezea
jinsi sekta yake pia imechomwa na janga hili.
Nyumbani pa mkahawa wa SOMA jijni Dar es Salaam |
Pia aliongezea kwamba ata vile vikundi vya usomjai
ndani ya shirika lake vimejikuta vikishindwa kuendelea kama kawaida. Kama vile
uga wa watoto ambao ulikaribisha watoto kujisomea. Pia kikundi chao cha vitabu
kinachoitwa ‘taswira’ ambacho kila mwezi huchagua vitabu vya waandishi tokea
Afrika na kujisomea kisha kuvichanmbua kwa pamoja. Kwa sasa wamebidi wakutane
mtandaoni na kikundi kama ‘taswira’ kimeshindwa kuagiza vitabu kupitia Soma kwa
urahisi.
Suluhu
kazi ya ubuifu ya Ailinda Sawe ndani ya Afrika Sana |
Japo changamoto ni nyingi kuna juhudi chanya zinazoleta
matumaini toka kwa wadau wa sekta hii. Kwa kuanzia na chama cha wabunifu wa
mavasi TAFDA ambao waliwakilisha TMDA-Tanzania Medicine & Medical Devices Authority’
mifano wa barakoa, kwenye taasisi hii ili kupata kibali. Ampabo saba kati yao
waliweza kufikia viwango na kupewa idhini ya kutengeneza barakoa zenye viwango
vya kimataifa ambazo zaweza tumiwa hadi hospitalini.
Bw Merinyo alitueleza na kuongezea kwa kuisii serikali
ndani ya mfuko wake wa maafa. Kuwaangalia wabunifu hawa ambao wana uwezo wa kutengeneza
nguo za kujikinga za kitaalam (PPE Suit) pale kwa idhini na TMDA. Wakipewa
ruzuku ya kujikita na uzalishaji kwani wengi wao wan a viwanda, wataweza
kutengeneza nguo hizi pamoja na barakoa zenye ubora wa uhakika kwa bei nafuu
nchini kote.
Wanadansi nao wamekuwa wakitumia kipindi hiki
kutengeneza mikanda nyongefu na kuitupa mitandaoni kama hapa T-Africa
Covid Dance. Waki isihi serikali na jamii kukumbuka kuwa tasnia yao inaweza
fikisha ujumbe kikamilifu; na vivyo wakumbukwe pale wasanii wanapohitajika
kusambaza ujumbe.
Kwenye tasnia ya usomaji wachapishaji wamekuwa
wakitumia fursa za kutangaza waandishi na vitabu vyao mitandaoni. Tukiona
waandishi wengi wakitumia muda huu kutotoa kazi za hadithi kuhusiana na kipindi
hiki, wanazo zisambaza mitandaoni na kuzitangaza kupitia vipindi vya redio kama
#KabatilaVitabu ndani ya boresha.online
Kwenye ulimwengu wa mziki, wanamziki wengi wamekuwa
wakitoa matamasha mitandaoni.
Mpiga guitar maarufu Norman Bikaka aliye na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye fani ya muziki wa jukwaani TZ |
Muda huu pia umewapa wasanii haswa wa mziki na filamu,
kufikiria k
wa upya umuhimu wa sheria ya hakimiliki kwenye kazi zao. Kwani sasa
sheria hii ilitakiwa iwawezeshe kupokea mirabaha kwa kazi zao popote zinapopigwa
pa hadhira (Bar, Vyombo vya Usafiri, Redio, Televisheni, Mitandaoni n.k.).
Tulipata fursa ya kumsikiliza Mkurugenzi Doreen Sinara wa COSOTA, ambaye
alituarifu kati ya kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu, shirika lake
lilitegemea kupokea mirabaha ya kufikia Tshs 336, 350,000/ toka kwa kazi za
wanachama wake.
Hadi sasa wameweza kukusanya kiasi cha Tshs 56,350,000/. Doren
alisema hawategemei kufikia malengo kwani janga hili la Corona limeathiri
sehemu za mikusanyiko kama vyombo vya usafiri, na sekta za huduma kama ma hoteli
na bar.
Kazi za wasanii wa kazi za mikono mkoani Arusha (picha courtsey) |
Kwa miaka nenda rudi vyombo vya habari Tanzania vimekuwa vikikwepa kulipa mirabaha kwa kazi za sanaa wanazorusha kwenye vipindi vyao. Japo sheria ya hakimiliki nchini copyright law No 7 of 1999 (RE 2019) inawa shindikiza kulipia kazi hizo. Mwaka huu Doreen alisema japo bado kuna changamoto kwenye ukusanyaji, COSOTA inategema hadi mwezi Juni 2020 kukusanya Tshs 51,000,000/kutoka kwa vyombo vya habari. Vivyo anawasihi wasanii kujisajili kama wanachama wa COSOTA, na pia kusajili kazi zao za sanaa wakitoa anuani zao za benki, ili waweze nufaika na mirabaha hii. Ambapo mwaka huu malipo ya nusu ya mwaka huu yatatolewa mwezi Agosti 2020.
Itakuwa jambo la busra kama janga hili litawashinikiza
wasanii kuwa na umoja na kusajili kazi zao na shirika hili, ili kuhakikisha
wanapata haki zao ata wasipokuwa jukwaani kama sasa. Vivyo kuwa na tabia ya
kusaini mikataba ya kulinda kazi zao, swala ambalo Doreen na Bw John Kitime
(msanii na muajiriwa wa awali wa COSOTA) walitueleza halizingatiwi na wasanii
wengi. Shirika hili huwa linatoa miongozo ya mikataba kwa sekta mbalimbali za
sanaa bure.
Bw Remitone mwanamziki na mjasiriamali kwenye tasnia ya muziki wa jukwaani Bongo. |
Vivyo wasanii hawa kupitia vyama vyao, wamependekeza
serikali itoe ruzuku ama mikopo nafuu kwa wasanii; kuwasaidia kuwekeza kwenye
kazi ndani ya kipindi hiki kigumu. Vivyo Dr Temu alisema kuwa serikali imekuwa
kwenye mchakato wa kuzindua mfuko wa utamaduni wa kuwasaidia wasanii. Pia wapo
kwenye mchakato wa kuandaa kanuni za kurejesha shughuli za jukwaani kwa wasanii.
Hapa tulipata dondoo toka kwa Bw Mngereza tokea BASATA kwamba mnamo tarehe 28
mwezi Mei, BASATA itakaa na wakuu wa mashirikisho ya sanaa nchini na kuwasikiliza
ili kujua taratibu gani iwape wizara.
Mchapishaji na Mkurugenzi wa Soma Book Cafe, Demere Kitunga |
Wakuu hawa akiwemo Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Wanamziki Bw John Kitime, alisema angependa kutumia fursa hii pia
kuishauri BASATA kuangalia jinsi ya kuimarisha mifumo ya vyama kwani wasanii wengi hawamo kwenye hivi vyama. Mawazo kama haya yanaungwa mkono na wasanii wengi ambao wamebaini Corona sio chanzo cha changamoto
kwenye kazi zao. Ila imefichua nyufa zilizokuwepo kwenye sekta yao na
vivyo wote kwa pamoja wanawajibu wa kuimarisha sekta yao.
No comments:
Post a Comment