Friday, 31 October 2014

Burudani na Sanaa Nov/Dec’14

By Sanaa & Culture

Siku zinaruka na hatimaye tunakaribia mwisho wa mwaka. Mwezi huu na ujao, tayari naona kuna mambo yaliyonona kwenye anga za Sanaa kwetu sote hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Wiki ijayo kuna tamasha la Muziki pale Bagamoyo ikijumuisha wanamziki wa TZ walionda shule. Kama kina Leo Mkanyia, Wahapahapa Band, Jhikoman, Vitalis Maembe na Msafiri Zawose.

Pia tarehe 7 Novemba Mzungu Kichaa amerudi nyumbani hivyo Beat Festival yaendelea ikiwa na Mopao Band, Malfred, na DJ toka UK David Tinning.

Bila kusahau bado maonyesho ya sanaa za mikono yazidi kupamba moto mwisho wa mwaka huu. We have fine art exhbits 'Blindfolded' still going on till december by Printmaker Gadi Ramadhan. Yeye ametafsiri kwenye sanaa zake za kutani (Monotypes/Monoprints) utamaduni wetu wa ububusa.


Ndani ya mada hii pia napendekeza ufwatilie onyesho la kina kaka Taye na Mutua toka Nigeria na Kenya liitwalo 'Africa is not a country', lilionaza rasmi Kenya na kuingia TZ na sasa linaenda nchi nyingine Africa. Nitatoa habari zake hapa MKEKA manake nilipata muwasho wa fikra wa kipekee kabisa, natumaini utakubaliana nami.

Kaka Minzi toka Mwanza naye anaonyesho liitwalo 'Shadow' pale Black Tomato mjini kati Dar es Salaam, Novemba. Kaka huyu anavyocheza na rangi ni balaa ‘simply’ balaa. Pia rafiki yake na mshawishi wa fikra kaka Vita Malulu ana onyesho lake la Sanaa mwezi wa Novemba kati, huyu kaka naye wakuangalia haswa kwa jinsi haogopi kutoa picha halisi ya jinsi Watanzania tunachukulia vitu poa wakati Wazee wetu wa nyuma na vizazi vya mbele vinatuangalia nini haswa twafanya kwenye historia. 

Pia mwisho wa Novemba kuna tamasha la utamaduni lijalo jijini Dar es Salaam pale Nafasi Artspace. Kwa jina la 'Marahaba Cultural Festival', kwa wale wapenzi wa Reggae na Maigizo. Vyema mwende kuchungulia, wasanii Segere Original, Jhikoman, Wahapahapa Band Fimbo Band, Parapanda Theatre, Seven Survivor, Cocoodo African Music, Mzungu Kichaa, Jipe Moyo Group na wengine wengi watatumbuiza.

Mwenyewe nina furaha kuwafahamisha nitatumbuizwa Novemba hii kwa nyimbo na shairi pale Club 327 ndani ya 'Lyricist Lounge'.

Desemba nayo si kavu japo ni mwezi mwisho, kuna onyesho la mavazi ‘Swahili Fashion Week’; filamu moto moto toka CDEA pale Mikocheni B as well party ya kufunga mwaka na bendi ya Wahapahapa pale Nafasi msikose...




Name of Event (Onyesho)
Place (Mahali)-Kiingilio (Entrance)
Date/Time (Muda,Siku)
Gadi Ramadhan-Art Exhibition ‘Blindfolded’
British Council DSM-Bure/Free
22Nd Oct-Dec’14
Chillax Halloween Party by Heinken
George & Dragon-DSM-Free
31.10.14-6pm/12 jioni
Chap Chap-Africa is not a Country na exhibition ‘Why Africans aren’t united’
Nafasi Artspace Mikocheni DSM-Free
1/11/14 4:30pm/!0:30 jioni
Onyesho la Sanaa za mikono ‘In and Out life stories’ by Ephrem Solomon na Jan Van Esch
Alliance Francais-DSM-Free/Bure
4/11/14 6:30pm/12:30 jioni
Sems Apparel-Grab a bag weekend (mwenzangu mwenyewe sina uhakika naona waweza pata begi)
Slipway-DSM
1st/2nd Nov’14-1 na 2 Novemba 12pm onwards Kuanzia Saa sita mchana
Karibu Music Festival
Mwanakalenge/Tasuba grounds-Bagamoyo Tshs5,000 kwa siku/per day au Tshs12,000 for 3 days/siku tatu
Tarehe 7 hadi 9 Novemba/7th-9th Nov’14. From 10am
Loyce Gayo’s Poetry Workshop and Performance
Alliance Francais-DSM-Free/Bure
5th na 19th Nov-6:30pm/12:30jioni
The Beat Festival
Triniti Bar Oysterbay-DSM Tshs 10,000
7/11/14 8pm/2usiku
Last Barazani of 2014
Alliance Francais-DSM-Bure/Free
12/11/14-7pm/1 usiku
Art Exhbition-Vita Malulu ‘Majangili’
Goethe Insitut-DSM-Free/Bure
13/11/14-6pm/12jioni
Fantuzzi & DJ Kaka-Global Troubador (Latin, Reggae, Funk) ni mtu na baba yake toka Puerto Rico si mchezo
Black Tomato Oysterbay Shopping Centre-DSM-Tshs 10,000
Novemba 15th 8pm/2 usiku hadi Novemba 16th 12:01am/6 usiku
Onyesho la Sanaa ya mikono ‘Tupo & The Magician’-Nadir Tharani
Alliance Francais-DSM-Free/Bure
18/11/14-6:30pm/12:30jioni
Onyesho la Sanaa za mikono ‘Shadow’ ya Minzi Thobias
Black Tomato-Mjini kati DSM-Bure/Free
20/11/14-7pm/1usiku
Filamu-Ma Mama nest Amerique (Mama yangu Mmarekani)
Alliance Francais-DSM-Bure/Free
22/11/14-11am/5 asubuhi
Lyricist Lounge (Sebleni kwa Malenga)
Club 327-Mikocheni, DSM-Free/Bure
22/11/14-7pm/1usiku
Dar Choral Society
Serena Hotel-DSM-30,000Tshs
23/11/14-6:30pm/12:30 jioni
‘CDEA’s Film Club’ yaonyesha filamu fupi ‘Otelo Burning’
CDEA’s HQ-Mikocheni B DSM-Free
28/11/14-6:30pm/12:30jioni
Marahaba Cultural Festival
Nafasi Artspace-DSM
29/11/14-$pm/10 jioni hadi 10pm/4 Usiku
Music Planet presents DJ Cartel vs DJ Senorita
Samaki Samaki Mjini kati/City Center-DSM-Free
29/11/14-9pm/3usiku
European Film Festival 2014
Alliance Francais, Goethe Institut, UDSM (Chuo cha Sanaa-FPA) in that order-Free
27, 28, 29/Novemba/14
Documentary Screening-‘Less is More’ filamu fupi
Alliance Francais-DSM-Free
3/12/14-7pm/1usiku
La Poetista (Featuring Masafa)
MOG (Iliyokuwa Nyumbani Lounge)-DSM-5K
4/12/14-7pm/1Usiku
MI Charity Concert Ft Mad Ice, Damien Soul, Grace Matata, MC Pilipili with guest artists Ben Pol & DJ Kaka Kahlil
Triniti Bar Oysterbay-DSM-10K
4/12/14-8pm-11am/2 usiku-5 usiku
Loyce Gayo presents Poetry/Dada wa Mistari Loyce apanda jukwaani
Alliance Francais-DSM-Free
5/12/14-6:30pm/12:30jioni
The Beat ikiwa na Ashimba, Abeneko na Sikinde
Triniti Bar Oysterbay-DSM-10K
5/12/14-8pm/2 usiku
Swahili Fashion Week
Hotel SeaCliff-DSM-(In advance-30K, Getini-40,000, VIP-70K)
5th-7th Dec’14
Filamu fupi-‘A Pakistani House Husband’ na Onyesho la Sanaa ya mikono
Alliance Francais-DSM
10/12/14-6:30pm/12:30 jioni
Open Show (Filamu fupi 5) of young film makers in Tanzania  
CDEA-ECO SANAA Mikocheni B-DSM-Free/Bure
18/12/14-7:00pm/1 usiku
THT-'Throw Down Thursday'
Ma DJ wanaovuma 
Black Tomato-Mjini DSM-Free
 18/12/14-4pm-8pm/10 jioni hadi 2 usiku
Party ya Kumaliza mwaka na Wahapahapa Band
Nafasi Artspace-Mikocheni, DSM
6:30pm-10pm/12:30 jioni-4 usiku

























2 comments:

  1. Thanks for keeping us in the know about all these great events happening in Dar :)

    ReplyDelete
  2. Shukrani, I am honored you appreciate it...

    ReplyDelete