Monday, 22 May 2017

Hazina za mimea asili ya fukwe za Afrika Mashariki


By +Caroline Anande Uliwa @CarolAnande-Instagram @CarolAnande-Facebook @CarolAnande-Twitter

Bi Shamba Ireen Colyvas Mtuil, ndani ya bustani
yake akiwa na miche ya Pembana, mmea asili
wa Afrika Mashariki
Athari za tabia nchi zinatukabili wa Afrika Mashariki kuliko tunavyodhani. Kwa wale wanaoishi ufukweni mwa Afrika Mashariki kuanzia Msumbiji (Mozambique) hadi Somali kusini, kupitia Tanzania na Kenya. Asimilia 90 ya mimea asilia inayoota humu ikihifadhi viumbe mbali mbali, (wengi wao wanaopatikana hapa tu duniani) imetoweka.

“Misitu ya fukwe za Afrika Mashariki pamoja na milima ya Uzungwa Tanzania yajulikana duniani na wanabiolojia, kama vyanzo pekee vya makazi ya viumbe wanaopatikana huku tu dunia nzima. Misitu ya pwani mabondeni inayo hifadhi watu kwa miaka nenda rudi (ma elfu) sasa imesalia kwa asimilia kumi tu…” Mazingira hatarini, Viumbe hatarini: Misitu na Pori za kanda ya fukwe za Afrika Mashariki hati ya WWF-World Wildlife Fund-2011

Changamoto


Wangapi tunoishi pwani tunagongana mitaani kwetu na miti kama Mkungu, Mvule au mimea ya Mabungo na Aloe-Memosa (aina ya aloe-vera asilia toka Afrika Mashariki). Haswa kwa wale tunaokaa miji ya Pwani za Afrika Mashariki, tunazidi sahau muonekano wa mimea hii. Kwani tumezungukwa na mimea geni kama miashok, miarobaini, ‘minazi ya njano’ n.k.

NIkiongea na Dkt William Joseph Kindeketa (Ph.D), afisa mtafiti wa viumbe hai pale Tanzania Commission for Science & Techonology-COSTECH. Alisema hali inazidi kudhofika licha ya baadhi ya misitu kutengwa kwa hifadhi, kama ‘Pande game reserve, Kazizungwi, Vitindu na Msitu wa Kusini Ruvu. 

Mti wa Mvule pale Bustani ya Botania jijini kati
Dar es Salaam, ni mti asilia ya fukwe za Afrika
Mashariki na upo hatarani kupotea 
“Mwaka 2016 hadi awali mwaka huu, nilifanya utafiti kujua maendeleo ya hifadhi hizi za misitu. Nilitembelea mikoa ya Pwani, Lindi na Dar es Salaam, nikaona wazi hali yazidi kuwa mbaya. Tokea juu na picha za ‘satelite’ huwezi ona vizuri hali ya misitu hii, ukiwa ndani ndo unaona uharibifu unaoendelea. Miti yakatwa kwa ajili ya biashara ya mkaa na mahitaji mengine ya watu licha ya kuwa sehemu pekee za hifadhi ya mazingira kitaifa, kama kule Ikwiliri, Rufiji”

http://www.ippmedia.com/sw/makala/ripoti-maalumuuvunaji-haramu-watishia-mikoko-kutoweka-nchini

Kuna manufaa mengi ya kuhifadhi na kuotesha mimea ya asili hata kwenye bustani zetu majumbani. Kwa kuwa mimea hii imeshazoea hali ya hewa ya maeneo yetu, huweza kustaimili kiangazi, pia kupunguza athari za mafuriko. Kwa kuwa inashamriri ina mtandao mkubwa wa mizizi chini ya ardhi, inayoshikilia ardhi na kunyonya maji vizuri toka kina cha chini. http://www.cardnonativeplantnursery.com/native-plants-seed/advantages-of-native-plants 

Pia mtandao huu husaidia kuchuja mchanga na kusaidia maji yanoyofika kwenye mito au visima kuwa safi, yakikosa mchanga na udongo mwingi. Vile vile kutosababisha mmonyoko wa ardhi. Mimea ya asili huwa imezoea wadudu waharibifu na wasionekana wa maeneo yao, vivyo huweza kukabiliana nao bila kutumia dawa kali za kemikali. Hata mbolea kwenye mimea hii haiitajiki kama kwenye mimea ngeni. 

Kwa kuwa mimea ya asili imekuwepo kwa miaka elfu na maelfu, wakuta imekua na kuelewana na viumbe hai wa sehemu ile. Pamoja na viumbe chavu kama nyuki na vipepeo, wengi wao wakipendelea kuishi kwenye mimea hii au kutumia maligafi yake kujikidhi. Vivyo ukitokomeza mmea wa asili ni kama umeondoa kijiji kizima, kwani wengi wa viumbe hawa hawawezi kuishi na mimea ngeni.

“Tulifanya tafiti kwenye kahawa za Kilimanjaro, tuliachia baadhi ya kahawa zikumbane na viumbe chavu na kahawa nyingine tulizinyima viumbe hawa. Mimea yote ilizaa, sema matunda ya zile kahawa zilizokosa viumbe chavu, yalikosa ubora ukilinganisha na kahawa zilizopewa viumbe chavu…”Dkt W. Kindeketa

Mifano ya suluhu


Dkt Anne Outwater mhadhiri wa chuo cha manesi Muhimbili-MUHAS, anayependa mno mazingira .https://www.safariadventures.club/home/category/Nature%20Notes Kwa sasa yupo kwenye mchakato akisaidiwa na Ilana Locker pamoja na Roy Gerau (wanabiologia wa bustani ya botania Missouri-USA) wa kuchapisha kitabu ‘Mimea Asili ya Fukwe za Afrika Mashariki’. Kitabu hiki kitatumia lugha zote mbili ikiwemo Kiswahili na Kingeresza. Kitaelezea zaidi mimea asilia ya fukwe za Afrika Mashairiki matunzo yake, jinsi ya kuiotesha n.k. https://www.linkedin.com/in/anne-h-outwater-71289927/?ppe=1
Shina la mnazi wa 'Pembana' ndani ya bustani
ya Bi Shamba Ireen Mtui 

Ikitoa majina na picha ya mimea hii kama Mkunga, Mkongo, Mujogolo, Mkuruti, Mtundu, Mkangazni, Mpwipwi, Mvule, Mswaki, Morula, Mluze, Mkwaju, Mbuyu, Mkuyu na mingine mingi. Pia itatoa elimu juu ya mimea geni iliyoteshwa kwenya kanda hii, na jinisi inavyoathiri mazingira yetu. 

Dkt. Anne pia alikuwa mmoja wa wanaharakati waliowezesha wanafunzi wa MUHAS awali mwaka huu. Kushirikiana na manispaa ya Ilala kwenye ‘wiki ya kusafisha ilala’ ambapo walisafisha pori la hifadhi ya Mikoko, karibu na Salendar Bridge jijini Dar es Salaam. Mansipaa baadaye ilimuomba awasaidie kutekeleza maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, itakayofanyika mwezi juni mwaka huu. https://youtu.be/C29DXB-Eyk0

Vivyo akamshirikisha rafiki yake Ireen Colyvas Mtui, ambaye ni Bi Shamba anayetunza na kuuza mimea mbalimbali tangu 1993. Bi Ireen ataipa manispaa ya Ilala zaidi ya miche 200, ili manispaa iipande siku hii ya mazingira duniani. Dkt Anne alitumia fursa hii ya kusaidia mazingira jijini DSM, kwa kujaribu kutengeneza akiba mbadala ya mnazi wa Pembana. Mnazi huu ulipewa tathmini mwaka 2009, kuwa hatarini kutoweka duniani na kitengo cha ‘East African Plant Red List Authority. http://www.palmpedia.net/wiki/Dypsis_pembana

Matawi ya mnazi wa Pembana ambao upo hatarani
kupotea na ni mti asilia wa fukwe za Afrika
Mashariki
Huu mnazi ni mmea asilia wa pwani ya Afrika Mashariki. Ukipatikana kisiwa cha Pemba pekee ndani ya msitu wa Ngezi mahala pasipozidi Kilometa 20 ‘square’. 

“Huu mnazi ni rahisi kuumudu, mbegu zake ni ndogo nyekundu. Kwa mwaka huzaa mara mbili hadi tatu. Anne alivyoniomba nimpe mbegu za mmea huu, nilihofu kama tutapata miche 200, kwani sikuwahi kuuza kwa wingi. Lakini nilichukua mbegu zake na kuzitupa ardhini, nilifurahi nlipoona zimechipua bila shida. Basi nikazihamisha kwenye vikopo. Baadaye zilivyozidi kuota nilihamisha mche mmoja, mmoja kwenda kwenye vyungu hivi unavyoviona vya plastiki…” Ireen Colyvas Mtui

Wanawake hawa wapo mstari wa mbele kukabiliana na janga hili linaokabili mimea yetu ya asili. Ukweli sio ajabu tunakabiliana na athari za tabia nchi, zinazoleta mvua bila mpangilio na joto au ukame usio wakawaidia, kurudisha mimea yetu asilia kutatusaidia kukumbana na tatizo hili. Hivyo ukiwa Dar es Salaam waweza fika kwenye bustani ya Mama Ireen pale Mlandege Rd, No7, Mikocheni B, Dar es Salaam-0713410857, ili na wewe ujipatie mmea wa asili na kusaidia mazingira yetu.

1 comment:

  1. Um drama que se estende a vários recantos de África.As opções erradas de desenvolvimento constituiem um dos dramas.E outro aspecto:as elites predadoras aliadas a interesses inconfessos.Estamos destruindo o que ainda nos resta de autenticidade e soberania.Importa que a sociedade civil seja de facto guardiã duma consciência ambiental.

    ReplyDelete