Wednesday 27 May 2020

Wadau wa Sanaa TZ na sokomoko la Covid-19


 By Caroline Uliwa

Wanadansi akwemo Tiko Mbepo ( mwisho kulia)
tokea Tanzania
“Yani hili janga likiisha wengine tutabidi tupimwe kisaikolojia, manake saa ingine unadhani una ugonjwa kumbe ni ‘stress’…”Remi Tone mwanamziki na mjasiriamali kwenye sekta ya muziki wa jukwani akijibu jinsi gani janga la Corona limeathiri kazi zake.
Tangu Corona itie mguu Tanzania mnamo mwezi Machi mwaka huu, sekta ya utamaduni na sanaa imeathirika kwa kiasi kikubwa. Hapa tumeongea na wadau mbali mbali kwenye sekta hii akiwemo Katibu Mtendaji wa BASATA Bw Godfrey Mngereza, na wasanii wasiopungua kumi ili kubaini hali halisi na suluhu gani zinazojitokeza kwa sekta hii kwa kipindi hiki.

Changamoto



“Ratiba yangu yote mwaka huu imetibuliwa ndani na nje ya nchi, nilikuwa natarajia kwenda kikazi mwaka huu South Afrika, Bolivia, Wingereza, Japan, Ghana na Eygpt ila mwishowe nilianza kuzoea ile barua pepe yenye ujumbe ‘Tunasikitika kukuarifu tumesitisha…” huwa nafundisha mashuleni  na kwa watu wazima ila hadi sasa hizi kazi pia zimesitishwa.” Dada Mwandale Mwanyekwa mwalimu na mkufunzi wa Sanaa ya ufundi hususani uchongaji wa vinyago alielezea.

Mwandale Mwanyekwa ama Big Mama mkali wa sanaa za ufundi TZ
Tulivyongea na Bw Robert Mwampemwa mkurugenzi wa chama cha wasanii wa ufundi ‘Tanzania Visual Artists Association’ yeye pia alishuhudia kuwa hali sio nzuri kwa wasanii wengine kwenye tasnia yake. Alisema kwa ajili sekta nyingi za uchumi zimeathirika kama vile utalii basi “Mnyororo wa uzalishaji umeathirika mno, mfikirie yule Mama Iringa anayesuka vikapu leo hii anashindwa kumuuzia yule mchukuzi aliyetoka mjini kwani yule haoni soko na vivyo hanunui kazi yake.” 
kazi ya dada Jamila Vera Swai mmoja wa
wanachama wa TFDA
Bwana Robert aliongezea kwa kusema vikundi vya uzalishaji wa hizi rasilimali za kazi za ufundi, wengi wao waliokuwa wakitoa ajira kwa vijana na watu wasiojiweza.Sasa wamebidi waachishe kazi wafanya kazi wao. Na kuwarejesha kwenye majaribio ya pombe na madawa ya kulevya.

Hili swala la kazi kukauka kwenye sekta hii lilikuwa jibu kutoka kwa wasanii wengi tuliongea nao hapa. Wengine wakiwa madansa, wanamuziki, wabunifu wa mavazi, wanafilamu. Swala la kusitishwa kwa mikusanyiko ya hadhara pia nchi ngeni kufunga mipaka yao ama kuwepo kwenye mifungo wa ndani yani ‘lockdowns’.

Kumeathiri wasanii kwa karibu kabisa “Ukisitisha matamasha, harusi, ‘kitchen party’, na hafla nyingine unaathiri biashara zetu moja kwa moja. Kwani hawa ni wateja wetu ambao wangeshona mavazi yao kwetu” Bw Ndesumbuko Merinyo mkongwe kwenye sekta ya ubunifu wa mavazi nchini, na jina la ‘Afrika Sana’; pia ni mkuu wa ‘Tanzania Fashion Designer Association-TAFDA tafda.org Alitujulisha hali halisi ya wanachama wake ndani ya tasnia hii, jinsi wanavyokabiliana na Corona. 

Aliongezea kwamba wengine wamebidi wawachishe mafundi wao kazi, kwani vyumba vya kazi walivyonavyo ni vidogo na kutokimu taratibu za kukaa mbali zinazopendekezwa kwenye kujitahadhari na Corona.
kazi ya Bw Thobias Minzi ama Minzi Mims mkufunzi na mmoja wa
wanachama wa TVAA
Madansa pia wameathirika kama mwana dansa Tiko Mbeko alivyotuarifu, yeye ni mkuu wa kikundi cha T-Africa tafricadancecrew. Na wao wamejikuta kazi zao ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam zikisitishwa.
Hata sekta ya uchapishaji nayo imeathrika, “Unajua pato limepungua kwa namna kadhaa kufikia hadi asilimia 80. Ndio hiki kitabu kipya  (Development as Rebellion-Wasifu wa Mh Julius K. Nyerere) kimetoa muamko kidogo. Ila mwishowe hatutegemei mauzo ya kitabu kimoja…kwa saa kuna watu wachache mjini ambako duka letu lipo” Mkuki Bgoya wa kampuni ya uchapishaji Mkuki na Nyota, wenye duka la vitabu TPH BookStore. Alielezea jinsi sekta yake pia imechomwa na janga hili.

Nyumbani pa mkahawa wa SOMA jijni Dar es Salaam
Pia wauzaji wengine wa vitabu nao wameshuhudia kazi kuathirika vibaya na janga hili wakiwemo Soma Book Café ambao pia wamejikuta wakipunguza wafanya kazi. “Pale sehemu halisi zikisitishwa, lazima tusogoee mtandaoni ila mabadiliko hayaji kwa uraisi na yanaitaji uwekezaji.” Mama Demere Kitunga Mkurugenzi wa sehemu hii alinisaidia kuelewa jinsi upungufu wa watu kudhuru sehemu za uga wa usomji kama yake, unavyoathiri tasnia yake.
Pia aliongezea kwamba ata vile vikundi vya usomjai ndani ya shirika lake vimejikuta vikishindwa kuendelea kama kawaida. Kama vile uga wa watoto ambao ulikaribisha watoto kujisomea. Pia kikundi chao cha vitabu kinachoitwa ‘taswira’ ambacho kila mwezi huchagua vitabu vya waandishi tokea Afrika na kujisomea kisha kuvichanmbua kwa pamoja. Kwa sasa wamebidi wakutane mtandaoni na kikundi kama ‘taswira’ kimeshindwa kuagiza vitabu kupitia Soma kwa urahisi.

Suluhu


kazi ya ubuifu ya Ailinda Sawe ndani ya Afrika Sana
Japo changamoto ni nyingi kuna juhudi chanya zinazoleta matumaini toka kwa wadau wa sekta hii. Kwa kuanzia na chama cha wabunifu wa mavasi TAFDA ambao waliwakilisha TMDA-Tanzania Medicine & Medical Devices Authority’ mifano wa barakoa, kwenye taasisi hii ili kupata kibali. Ampabo saba kati yao waliweza kufikia viwango na kupewa idhini ya kutengeneza barakoa zenye viwango vya kimataifa ambazo zaweza tumiwa hadi hospitalini.

Bw Merinyo alitueleza na kuongezea kwa kuisii serikali ndani ya mfuko wake wa maafa. Kuwaangalia wabunifu hawa ambao wana uwezo wa kutengeneza nguo za kujikinga za kitaalam (PPE Suit) pale kwa idhini na TMDA. Wakipewa ruzuku ya kujikita na uzalishaji kwani wengi wao wana viwanda, wataweza kutengeneza nguo hizi pamoja na barakoa zenye ubora wa uhakika kwa bei nafuu nchini kote.  

Wanadansi nao wamekuwa wakitumia kipindi hiki kutengeneza mikanda nyongefu na kuitupa mitandaoni kama hapa  T-Africa Covid Dance. Waki isihi serikali na jamii kukumbuka kuwa tasnia yao inaweza fikisha ujumbe kikamilifu; na vivyo wakumbukwe pale wasanii wanapohitajika kusambaza ujumbe.

Kwenye tasnia ya usomaji wachapishaji wamekuwa wakitumia fursa za kutangaza waandishi na vitabu vyao mitandaoni. Tukiona waandishi wengi wakitumia muda huu kutotoa kazi za hadithi kuhusiana na kipindi hiki, wanazo zisambaza mitandaoni na kuzitangaza kupitia vipindi vya redio kama #KabatilaVitabu ndani ya boresha.online
Kwenye ulimwengu wa mziki, wanamziki wengi wamekuwa wakitoa matamasha mitandaoni. 

Mpiga guitar maarufu Norman Bikaka
aliye na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye
fani ya muziki wa jukwaani TZ
Pia haswa wale wa bongo flava wamekuwa wakizidi tangaza kazi zao kwenye maredio na televisheni na kunyakua mirabaha kwenye mitandao kama YouTube. Japo ufadhili wa matamasha haya mitandaoni si mkubwa ila mashirika kama Alliance Francais na MTV ambao tamasha lao hivi karibuni pa siku ya Afrika duniani AfricaDayBenefitConcert lilitoa ajira kwa wasanii mbalimbali kama Diamond Platnums wa TZ. Pia kazi zilizopo kwenye  tovuti ‘streaming’ kama bandcamp zimekuwa zikiuza miziki kwa wingi, vivyo wanamziki wenye kazi zao humu wamekuwa wakipata ahweni.

Muda huu pia umewapa wasanii haswa wa mziki na filamu, kufikiria k
wa upya umuhimu wa sheria ya hakimiliki kwenye kazi zao. Kwani sasa sheria hii ilitakiwa iwawezeshe kupokea mirabaha kwa kazi zao popote zinapopigwa pa hadhira (Bar, Vyombo vya Usafiri, Redio, Televisheni, Mitandaoni n.k.). Tulipata fursa ya kumsikiliza Mkurugenzi Doreen Sinara wa COSOTA, ambaye alituarifu kati ya kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu, shirika lake lilitegemea kupokea mirabaha ya kufikia Tshs 336, 350,000/ toka kwa kazi za wanachama wake. 

Hadi sasa wameweza kukusanya kiasi cha Tshs 56,350,000/. Doren alisema hawategemei kufikia malengo kwani janga hili la Corona limeathiri sehemu za mikusanyiko kama vyombo vya usafiri, na sekta za huduma kama ma hoteli na bar.
Kazi za wasanii wa kazi za mikono mkoani Arusha (picha courtsey)

Kwa miaka nenda rudi vyombo vya habari Tanzania vimekuwa vikikwepa kulipa mirabaha kwa kazi za sanaa wanazorusha kwenye vipindi vyao. Japo sheria ya hakimiliki nchini copyright law No 7 of 1999 (RE 2019) inawa shindikiza kulipia kazi hizo. Mwaka huu Doreen alisema japo bado kuna changamoto kwenye ukusanyaji, COSOTA inategema hadi mwezi Juni 2020 kukusanya Tshs 51,000,000/kutoka kwa vyombo vya habari. Vivyo anawasihi wasanii kujisajili kama wanachama wa COSOTA, na pia kusajili kazi zao za sanaa wakitoa anuani zao za benki, ili waweze nufaika na mirabaha hii. Ambapo mwaka huu malipo ya nusu ya mwaka huu yatatolewa mwezi Agosti 2020.

Itakuwa jambo la busra kama janga hili litawashinikiza wasanii kuwa na umoja na kusajili kazi zao na shirika hili, ili kuhakikisha wanapata haki zao ata wasipokuwa jukwaani kama sasa. Vivyo kuwa na tabia ya kusaini mikataba ya kulinda kazi zao, swala ambalo Doreen na Bw John Kitime (msanii na muajiriwa wa awali wa COSOTA) walitueleza halizingatiwi na wasanii wengi. Shirika hili huwa linatoa miongozo ya mikataba kwa sekta mbalimbali za sanaa bure.

Bw Remitone mwanamziki na mjasiriamali kwenye tasnia ya muziki
wa jukwaani Bongo
.
Kwa kukabiliana na changamoto za janga hili, wasanii wamekuwa wakikutana mitandaoni kupitia ‘apps’ kama Zoom na kupeana ushauri. Nlipata fursa ya kushiriki kwenye mikutano rasmi kama hii miwili. Iliyofadhiliwa na CDEA-culture & Development East Africa na Unleashed Africa. Mikutano hii imekuwa ikitoa manufaa makubwa kwa kuwakutanisha wasanii na wadao wengine kwenye sekta kama Dk Emmanuel Temu Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo kwenye Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Ambaye alipokea mirejesho kutoka kwa wasanii mbalimbali na kuahidi kuiwasilisha wizarani.

Vivyo wasanii hawa kupitia vyama vyao, wamependekeza serikali itoe ruzuku ama mikopo nafuu kwa wasanii; kuwasaidia kuwekeza kwenye kazi ndani ya kipindi hiki kigumu. Vivyo Dr Temu alisema kuwa serikali imekuwa kwenye mchakato wa kuzindua mfuko wa utamaduni wa kuwasaidia wasanii. Pia wapo kwenye mchakato wa kuandaa kanuni za kurejesha shughuli za jukwaani kwa wasanii. Hapa tulipata dondoo toka kwa Bw Mngereza tokea BASATA kwamba mnamo tarehe 28 mwezi Mei, BASATA itakaa na wakuu wa mashirikisho ya sanaa nchini na kuwasikiliza ili kujua taratibu gani iwape wizara.
Mchapishaji na Mkurugenzi wa Soma Book Cafe, Demere Kitunga
Mapendekezo ya jinsi gani ya kufungua shughuli za sanaa kwa hadhira kwa namna salama na endelevu. 

Wakuu hawa akiwemo Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wanamziki Bw John Kitime, alisema angependa kutumia fursa hii pia kuishauri BASATA kuangalia jinsi ya kuimarisha mifumo ya vyama kwani wasanii wengi hawamo kwenye hivi vyama. Mawazo kama haya yanaungwa mkono na wasanii wengi ambao wamebaini Corona sio chanzo cha changamoto kwenye kazi zao. Ila imefichua nyufa zilizokuwepo kwenye sekta yao na vivyo  wote kwa pamoja wanawajibu wa kuimarisha sekta yao. 


No comments:

Post a Comment